|
AZIMIO LA WANAWAKE KATIKA MUZIKI – ROMA, SEPTEMBA 2000
Mwishoni mwa
kongamano la kwanza la kimataifa “Donne in Musica Gli Incontri al
Borg, Fiuggi” mwaka wa 1996, wanamuziki wa kike kutoka inchi
ishirini na sita “26” ukijumuisha watungaji, wasanii, viongozi,
wasomi wa muziki na watayarishaji, waliithinisha stakabathi
ijulikanayo “Azimio La Fiuggi 1996”.
Azimio hili ambalo
limesambazwa kote duniani kwa wanawake katika mashirika ya muziki na
usomi, huangazia yale amboyo ni malengo ya musingi kulingana na
wanamuziki wa kike.
Munamo mwaka wa 1999, azimio hili lilifanywa
marekebisho na kukubaliwa kwa umoja munamo September 2000. Hii
ilifatiwa na kukubaliwa na kamati ya wakfu wa utunzaji katika Roma.
Stakabadhi hii, inajumuisha yafuatayo:
Kila inchi inakaribishwa
kuendeleza uundaji wa mashirika ya kutoa stakabadhi na habari kuhusu
wanawake watungaji na mipaka yao ya kitaifa. Mashirika haya lazima
yaweze kutoa na kupata habari kuhusu wanamuziki wakike hasa katika
usambazaji na utoaji wa muziki. Tamasha za muziki wa kisasa na
wakale, tamasha za kuhusisha wanawake pekee, uwezekano wa
kufadhiliwa na kudhaminiwa kwa masomo ya wanawake wapewe kipao mbele
katika utoaji na uenezaji wa muziki ili kuongoza ujuzi katika muziki.
Wanawake wachukue nafasi ya kwanza katika uandaaji wa muziki katika
inchi zao na kuendeleza uhusiano kati ya watungaji na wasanii.
Mashirika haya yaweza kuunganishwa kupitia mutandao “WWW”. Utungaji
wa sheria katika inchi nyingi huwapa wanawake nafasi sawa na haki
kimawazo na lazima pia wapewe nafasi sawa katika nyanja zote za
kujiendeleza. Katika utendaji, hili huwa sivio. Wanawake katika
makundi ya muziki lazima waone kama maisha ya jamii yanaenda
sambamba na sheria zilizoko. Katika inchi nyingi wanawake
hawajawakilishwa ipasavyo katika tahasisi hizi. Lazima tuhakikishe
kua, wanawake wanashirikishwa kwenye majopo na kamati na sehemu
zingine ambapo talanta zao zahitajika.
Wanasiasa wanawake lazima
wafahamu tofauti zilizoko baina ya uundaji sheria na utekelezaji na
wapiganie kwa niaba ya wanamuziki wa kike kupata ufadhili. Habari
kuhusu wanamuziki wakike lazima zipewe kwa walimu wa muziki wake kwa
waume. Majukumu yanayotekelezwa na wanawake katika muziki lazima
yajumuishwe kwa ratiba ya masomo katika shule, viuo na viuo vikuu.
Wazazi nao wasaidie watoto wao waschana kwa wavulana kutambua na
kuendeleza vipawa viao katika muziki. Hii itasaidia kujivunia
nakuendeleza itikadi na utamaduni wao. Wanamuziki wa kike
wanahimizwa kusoma, kujipa mwoyo na watumie sitakabadhi ya shirika
la umoja wamataifa linalo husika na maswala ya elimu, sayanzi na
utamaduni “UNESCO” kuhusu haki za musanii na sitakabadhi ya mwisho
kutoka kwa kongamano la serikali kuhusu sera za kitamaduni ulio
fanywa Stockoholm mwak wa 1998. Juhudi za wanawake katika utamaduni
na maendeleo, yafaa yaangaziwe na washirikishwa kwenye uandaji wa
sera za kitamaduni katika nyanja zote. Hatuna budi kuhifadhi,
kuendeleza na kutetea talanta za usanii wa wanawake katika jamii.
Hii ndio njia pekee ya kushinda zana za ubaguzi wa utamaduni zilizo
buniwa na wanaume. Jukumu letu katika kuangazia maswala bayana na
yasio bayana hayawezi kupuuzwa kwasababu hayahusu tu watu au
utamaduni, bali pia ubinadamu kwa ujumula. |